Sunday, July 13, 2014

KOMBE LA DUNIA 2014: UJERUMANI MABINGWA WAPYA WA DUNIA, MESSI AFUTA MACHOZI NA TUZO YA MCHEZAJI BORA WA MASHINDANO.

HATIMAYE michuano ya Kombe la Dunia iliyokuwa inafanyika nchini Brazil imefikia kilele jana usiku kwa Ujerumani kutangazwa mabingwa wapya wa michuano hiyo baada ya kuifunga Argentina katika mchezo wa fainali uliofanyika Uwanja wa Maracana jijini Rio de janeiro. Katika mchezo huo ambao ulikwenda mpaka muda wa nyongeza kutokana na timu hizo kushindwa kufungana kwa muda wa kawaida, Ujerumani walifanikiwa kupata bao lao pekee katika mchezo huo kupitia kwa Mario Gotze katika dakika ya 113. Ujerumani mbali na kunyakuwa taji hilo lakini pia golikipa wake Manuel Neuer alitunukiwa tuzo ya kipa bora wa mashindano hayo huku mshambuliaji wa Colombia James Rodriguez akiondoka na kiatu cha dhahabu kw akufunga mabao sita. Mshindi wa tuzo nne za Ballon d’Or na mshambuliaji wa Argentina na klabu ya Barcelona, Lionel Messi yeye ameibuka mchezaji bora wa mashindano hayo na kutunukiwa tuzo ya mpira wa dhahabu.

No comments:

Post a Comment