Wednesday, July 16, 2014

LANGALANGA: MARCEDES YAMUONGEZEA MKATABA ROSBERG.

TIMU ya magari ya langalanga ya Marcedes imethibitisha kumuongeza mkataba mwingine dereva wake nyta Nico Rosberg. Rosberg raia wa Ujerumani kwasasa anaongoza katika msimamo wa mbio za ubingwa wa dunia akimpita dereva mwenzake Lewis Hamilton raia wa Uingereza. Akihojiwa Rosberg amesema imekuwa ni safari ngumu kufika mahali walipo lakini kila mtu amekuwa akiwaamini na kutoka na ushirikiano wanaopewa na Marcedes-Benz kwasasa wanaongoza mbio hizo za langalanga. Rosberg dereva wa zamani wa timu ya Williams alijiunga na Marcedes mwaka 2010 ambapo mpaka sasa ameshashinda mashindano sita ya Grand Prix, matatu kati ya hayo akishinda msimu huu.

No comments:

Post a Comment