Friday, July 11, 2014

LIVERPOOL YAKUBALI KUMUACHIA MTUKUTU SUAREZ.

HATIMAYE klabu ya Liverpool imekubali kumuuza mshambuliaji Luis Suarez kwenda Barcelona kwa mkataba wa miaka mitano na kuwafanya kuvuna kitita cha paundi milioni 75. Mshambuliaji huyo wa kimataifa wa Uruguay mwenye umri wa miaka 27 kwasasa anatumikia kifungo cha miezi minne alichopewa na Shirikisho la Soka Duniani-FIFA kwa kosa la kumng’ata beki wa Italia Giorgio Chiellini katika michuano ya Kombe la Dunia. Suarez ambaye alishinda tuzo ya mchezaji wa bora wa mwaka nchini Uingereza mwaka jana baada ya kufunga mabao 31 katika ligi anatarajiwa kusafiri kwenda nchini Hispania wiki ijayo kwa ajili ya vipimo vya afya. Nyota huyo amewaandikia barua ya wazi mashabiki wa Liverpool kwa kumheshimu na kumvumilia katika kipindi chote alichokuwa Anfield huku pia akiwashukuru wachezaji, viongozi na benchi zima la ufundi la timu hiyo kwa ushirikiano waliokuwa wakimpa. Suarez amesema kwa moyo mzito anaiacha klabu hiyo na kwenda kutafuta changamoto mpya nchini Hispania lakini kamwe hawezi kuisahai timu hiyo hususani mashabiki wake kwa ushirikiano mkubwa waliompa katika kipindi chote.

No comments:

Post a Comment