Thursday, July 17, 2014

LIVERPOOL YAMKOMALIA BONY.

KLABU ya Liverpool imeonyesha utayari wa kuongeza ofa yao kwa ajili ya kumsajili kiungo wa timu ya Swansea City Wilfried Bony wakiwa wanataka kuendelea kuimarisha kikosi chao kwa ajili ya msimu wa 2014-2015. Swansea wanaonekana kutaka kiasi cha paundi milioni 19 kwa Liverpool ambao wana fedha za kutumia kutokana na mauzo ya Luis Suarez kwenda Barcelona waliyovuna kiasi cha paundi milioni 75. Mara ya kwanza Liverpool walitaka kutoa kiasi cha paundi milioni 12.5 kwa ajili ya nyota huyo wa kimataifa wa Ivory Coast lakini sasa wapo tayari kupandisha dau hilo mpaka kufikia paundi milioni 15. Bony ambaye ameifungia nchi yake mabao mawili katika michuano ya Kombe la Dunia na kuongeza mengine 26 aliyofunga kwa klabu yake katika msimu wa 2013-2014, pia amekuwa akiwindwa na Tottenham Hotspurs.

No comments:

Post a Comment