Tuesday, July 15, 2014

MARKOVIC AKAMILISHA USAJILI WAKE LIVERPOOL.

NYOTA wa kimataifa wa Serbia Lazar Markovic amethibitisha kuwa anatarajia kuwa mchezaji mpya wa Liverpool baada ya kutuma picha katika ukurasa wake wa mtandao wa kijamii wa facebook. Jumamosi kulikuwa na taarifa kuwa Markovic alisafiri kutoka jijini Lisbon kwenda kufanyiwa vipimo vya afya na kumalizia hatua za mwisho za uhamisho utakaogharimu kitita cha euro milioni 25 kutoka Benfica. Sasa nyota huyo amebainisha kuwa dili hilo tayari limekwishafanikiwa kwa kutuma picha yak wake mwenyewe akiwa ameshika jezi ya Liverpool, akisaliamiana na mashabiki na kufanya mahojiano yake ya kwanza na luninga ya klabu hiyo. Markovic anakuwa mchezaji wa nne kusajiliwa na Liverpool katika kipindi cha usajili wa majira ya kiangazi baada ya kusajiliwa kwa Rickie Lambert na Adam Lallana kutoka Southampton na kiungo wa Bayer Liverkusen Emre Can.

No comments:

Post a Comment