KLABU ya Chelsea imejiweka katika nafasi nzuri ya kumsajili kiungo wa Real Madrid Sami Khedira baada ya jana usiku wakala wake kudai kuwa hakuna makubaliano yaliyofikiwa na Arsenal. Meneja wa Chelsea, Jose Mourinho ambaye tayari amemsajili beki wa kushoto Filipe Luis kutoka Atletico Madrid kwa paundi milioni 18 na sasa anaweza kuhamishia nguvu zake kwa kiungo huyo wa kimataifa wa Ujerumani. Mara ya kwanza ilifahamika kuwa Arsenal ilikubali kutoa kitita cha paundi milioni 20 kwa Madrid kumnunua mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 27, lakini walikuwa wanasuasua kufika kiwango cha mshahara anaotaka wa paundi 180,000 kwa wiki. Hata hivyo, wakala wa Khedira, Jorg Neubauer amesema hawako katika mazungumzo na Arsenal na hafikirii kama wanaweza kukubaliana ada kwasababu wangeambiwa.

No comments:
Post a Comment