Thursday, July 17, 2014

PACQUIAO KUZICHAPA NOVEMBA.

BONDIA mahiri kutoka Phillipens, Manny Pacquiao ametangaza pambano lake litakalofuata kuwa ni dhidi ya bondia asiyepigika Chris Algieri kutoka Marekani. Pacquiao ambaye anashikilia mkataba wa dunia wa WBO uzito wa welter anatarajiwa kupambana na bondia huyo Novemba 22 huko Macau, China. Algieri ambaye alikuwa mchezaji wa zamani wa kick-boxer, alifuzu kucheza pambano hilo baada ya kumtandika Ruslan Provodnikov katika pambano lililofanyika mwezi uliopita. Mara ya mwisho Pacquiao kupigana ilikuwa ni April mwaka huu wakati alipomtandika Timothy Bladley katika pambano lililofanyika Las Vegas, Marekani.

No comments:

Post a Comment