Tuesday, July 15, 2014

RAIS WA ARGENTINA AUSHANGAZA ULIMWENGU KWA KUDAI HAKUTIZAMA MECHI HATA MOJA YA NCHI YAKE KATIKA KOMBE LA DUNIA IKIWEMO YA FAINALI.

RAIS wa Argentina, mwanamama Cristina Fernandez amekiri jana kuwa hakutizama mechi hata moja ya nchi yake katika michuano ya Kombe la Dunia ukiwemo mchezo wa fainali. Siku moja baada ya taifa hilo lenye mapenzi makubwa na soka kufugwa bao 1-0 na Ujerumani katika mchezo fainali, rais huyo aliipokea timu hiyo katika mji mkuu na kuwakumbatia wachezaji walioonekana kuwa na huzuni kwa kushindwa kurudi na kombe. Fernandez alikataa mwaliko wa rais wa Brazil Dilma Rousseff kuhudhuria mchezo wa fainali kwa madai ya kuuza koo lake lakini mwenzake wa Ujerumani Kansela Angela Markel alihudhuria mchezo huo huku akiruka kwa furaha wakati lilipofunga bao la ushindi. Akitoa hotuba yake mbele ya kikosi hicho kilichokuwa kikiongozwa na Lionel Messi, Fernandez amesema kuwa yeye sio mshabiki wa soka na hakutizama hata mchezo mmoja ukiwemo wa fainali na kudai kuwa ilibaki kidogo ampigie siku kocha Alejandro Sabella kwa kudhani kuwa wameshinda taji. Ingawa kauli ya rais huyo haikuwashangaza sana watu wan chi hiyo kutokana na kumfahamu rais huyo kwa tabia yake ya kutopenda michezo lakini amekosolewa vikali kwa kushindwa kuonyesha kujali hata kidogo wakati taifa hilo likiwa katika majonzi ya kufungwa.

No comments:

Post a Comment