KLABU ya Bayern Munich imetangaza kuwa Tony Kroos amekamilisha uhamisho wake kwenda Real Madrid kwa ada ambayo hawakuiweka wazi. Kiungo huyo mshambuliaji amekuwa akihusishwa kwa kipindi kirefu kuhamia kwa mabingwa hao wa Ligi ya Mabingwa barani Ulaya na sasa amesaini mkataba utakaomuweka Madrid mpaka mwaka 2020. Ofisa mkuu wa Bayern, Karl-Heinz Rummenigge alimshukuru nyota huyo kwa muda wake wote aliochezea timu hiyo na kumtakia heri yeye na familia katika maisha mapya huko Hispania. Bayern walikuwa wakitaka kumbakisha nyota huyo mwenye umri wa miaka 24 lakini walilazimika kumuweka sokoni baada ya kushindwa kufikia makubaliano juu ya mkataba mpya.

No comments:
Post a Comment