KOCHA wa zamani wa kikosi cha kwanza cha Manchester United, Rene Meulensteen amesisitiza Louis van Gaal atahitaji muda ili aweze kujitengenezea jina lake Old Trafford. Kocha huyo mwenye umri wa miaka 62 anatarajiwa kuanza kibarua chake United kesho kufuatia kuiwezesha Uholanzi kushika nafasi ya tatu katika michuano ya Kombe la Dunia iliyomalizika nchini Brazil Jumapili iliyopita. Meulensteen ambaye alikaa United kwa misimu 12 akiwa chini ya Sir Alex Ferguson, aliondoka muda mfupi mara baada ya David Moyes kutua klabuni hapo. Kocha huyo amesema United kwasasa inapitia mabadiliko makubwa kutokana na baadhi wachezaji wake kustaafu na wengine kuondoka hivyo lazima Van Gaal atahitaji muda ili kuweza kukiunganisha tena kikosi hicho na kuzoea mfumo wake wa uchezaji.

No comments:
Post a Comment