WALCOTT NJIANI KUREJEA UWANJANI.
WINGA mahiri wa klabu ya Arsenal, Theo Walcott bado ana matumaini ya kupona mapema majeruhi ya goti kwa kudokeza kuwa anakaribia kurejea katika kikosi cha kwanza. Walcott aliumia goti katika mchezo wa Kombe la FA walioshinda mabao 2-1 dhidi ya Tottenham Hotspurs Januari mwaka huu iliyopelekea kukosa msimu uliosali sambamba na michuano ya Kombe la Dunia iliyomalizika juzi nchini Brazil. Ingawa nyota huyo mwenye umri wa miaka 25 anafurahia kupona kwake ameamua kutokutoa tarehe haswa atakayorejea uwanjani. Walcott aluambia mtandao wa klabu hiyo kuwa kwasasa mambo yake yanakwenda vyema kwani amekuwa akifanya bidii katika kipindi chote hiki cha kiangazi kuhakikisha anarejea katika hali yake ya kawaida.
No comments:
Post a Comment