MENEJA wa klabu ya Arsenal, Arsene Wenger ana uhakika wa kukamilisha uhamisho wa mshambuliaji wa Barcelona Alexis Sanchez na wachezaji wengine wawili wanaweza kufuata kwa kutumia kikita cha paundi milioni 50. Nyota huyo wa kimataifa wa Chile amekubali kutua Arsenal badala ya Liverpool na Juventus na wawakilishi wake tayari wako jijini London kufikia makubaliano binafsi ili kukamilisha uhamisho huo. Inaaminika kuwa Sanchez atakuwa kilipwa mshahara sawa na anaolipwa Mesut Ozil wa paundi 140,000 kwa wiki na Arsenal inatarajiw akuwalipa Barcelona paundi milioni 30 ili waweze kumamilisha uhamisho wa mshambuliaji wa Liverpool Luis Suarez wa paundi milioni 75. Arsenal pia inatarajia kukamilisha uhamisho wa beki wa Newcastle United Mathieu Debuchy utakaowagharimu kiasi cha paundi milioni 11 huku uhamisho wa mshambuliaji wa Queens Park Rangers Loic Remy wa paundi milioni nane ukiwa umekwamishwa na mambo binafsi. Debuchy atakuwa mbadala wa Bacary Sagna katika nafasi ya beki wa kulia ambaye aliondoka Gunners na kutimkia Manchester City.

No comments:
Post a Comment