Wednesday, July 16, 2014

WEST HAM YAMNASA VALENCIA.

MSHAMBULIAJI wa kimataifa wa Ecuador, Enner Valencia amefikia makubaliano binafsi na klabu ya West Ham United ili asajiliwe rasmi Upton Park. Meneja wa West Ham amekuwa katika mikakati mizito ya kuimarisha safu yake ya ushambuliaji katika msimu wa 2014-2015 na Valencia ameonekana kama chaguo lake sahihi. Inadaiwa kuwa West Ham imekubali kutoa kitita cha paundi milioni 15 kwa timu ya Pachuca ya Mexico huku wakimpa Velencia mkataba wa miaka mitano. Mapema rais wa Pachuca Jesus Martinez alikaririwa akisisitiza kuwa nyota huyo hataweza kuondoka chini ya kiwnago hicho cha fedha ambacho kinavunja rekodi kwa kuwa kikubwa zaidi katika uhamisho kwenye soka la Mexico. Valencia mwenye umri wa miaka 25 ndiye aliyefunga mabao yote matatu kwa timu yake ya taifa ya Ecuador katika michuano ya Kombe la Dunia iliyomalizika mwishoni mwa wiki iliyopita nchini Brazil.

No comments:

Post a Comment