KLABU ya FC Copenhagen ya Denmark imethibitisha kuwa katika mzungumzo na Leicester City kwa ajili ya kumsajili nyota wa kimataifa wa Ghana Daniel Amartey. Vyombo vya habari vimeripoti kuwa Leicester ambao wanashikilia nafasi ya pili katika msimamo wa Ligi Kuu nyuma ya Arsenal kwa tofauti ya magoli, wametoa ofa ya dola milioni 8.73 kwa ajili ya kiungo huyo mwenye umri wa miaka 21. Kufuatia tetesi hizo, klabu hiyo ilithibitisha kuwepo katika mazungumzo na Leicester lakini hakuna lolote lililoafikiwa mpaka sasa. Amartey alijiunga na FC Copenhagen Julai mwaka 2014 akitokea klabu ya Djurgarden ya Sweden mwaka 2013.

No comments:
Post a Comment