Wednesday, January 13, 2016

WAHUNI WACHORA JINA LA MESSI KATIKA SANAMU LA RONALDO.

VYOMBO vya habari nchini Ureno, vimeripoti kuwa sanamu la Cristiano Ronaldo lililopo huko Fanchal, mji mkuu wa kisiwa cha Madeira liliamiwa na wahuni na kupakwa rangi ya jina na namba anayovaa Lionel Messi. Tukio linadaiwa kufanyika usiku wa kuamkia Jumanne, saa chache baada ya nyota huyo wa kimataifa wa Agentina na Barcelona kutwaa tuzo yake ya tano ya mchezaji bora wa mwaka wa dunia maarufu kama Ballon d’Or akimshinda Ronaldo. Jina la Messi pamoja namba 10 zote zilichorwa kwa rangi nyekundu katika sanamu hilo kabla ya wahusika kwenda kusafisha sanamu hilo na kufuta kilichoandikwa. Akihojiwa dada yake Ronaldo, Katia Aveiro amesema tukio hilo ni la aibuna linaonyesha jinsi wanamuonea wivu ndugu yake huyo. Ronaldo alizindua sanamu hilo la shaba lenye urefu wa mita 3.40 Desemba mwaka 2014, mita chache kutoka katika makumbusho yake mwenyewe aliyotengeneza katika mji huo.

No comments:

Post a Comment