MENEJA wa mpya wa Real Madrid, Zinedine Zidane anataka kumfanya Paul Pogba kuwa usajili wake wa kwanza toka apewe mikoba ya kuinoa klabu hiyo. Zidane mwenyewe alihama kutoka Juventus na kutua Santiago Bernabeu mwaka 2001 enzi hizo akiwa mchezaji na sasa anataka Mfaransa mwenzake huyo kufuata nyayo zake. Hata hivyo, suala hilo halitakuwa rahisi kwani mahasimu wao Barcelona na pia wanamuwania kiungo huyo. Ujumbe maalumu wa Madrid uliongozwa na Ariedo Braida na Albert Soler ulisafiri kuelekea jijini Turin kiangazi mwaka jana kufanya mazungumzo na Juventus kuhusu Pogba. Kipindi hicho walikuwa wamefungiwa kusajili hivyo walishindwa kukamilisha dili hilo wakati klabu pia ilishindw akutoa kitita kilichohitajika na Juventus kwa ajili ya nyota huyo mwenye umri wa miaka 22. Tatizo kubwa linaikabili Madrid hivi sasa ni uhusiano usio mzuri na wakala wa mchezaji huyo Mino Raiola ambao uliharibika kufuatia Carlo Ancelotti kupinga usajili wa Pogba.

No comments:
Post a Comment