Monday, March 14, 2016

OFISA SAFA AFUNGIWA NA FIFA.

KAMATI ya maadili ya Shirikisho la Soka Duniani-FIFA leo imemfungia ofisa wa zamani wa Chama cha Soka cha Afrika Kusini-SAFA, Leslie Sedibe kwa miaka mitano baada ya kukutwa na hatia ya kuhusika na upangaji matokeo wa timu ya taifa. Sedibe ambaye alikuwa ofisa mkuu wa SAFA kwa mwaka mmoja ikiwemo katika michuano ya Kombe la Dunia mwaka 2010 wakati nchi hiyo ikiwa mwenyeji, pia ametozwa faini ya dola 20,000. Waamuzi wa zamani wawili, Steve Goddard na Adeel Carelse nao pia wamefungiwa miaka miwili na kamati hiyo ya FIFA. Inadaiwa kuwa walipanga matokeo katika mechi za kimataifa za kirafiki ambazo zilichezwa Afrika Kusini mwaka 2010 kabla ya michuano ya Kombe la Dunia.

No comments:

Post a Comment