MENEJA wa Tottenham Hotspurs, Mauricio Pochettino amefanikiwa kutwaa tuzo ya Meneja Bora wa mwezi baada ya kukiongoza kikosi chake kushinda mechi nne mfululizo mwezi uliopita. Ushindi dhidi ya Watford, Swansea City, Norwich City na ule wa mkubwa wa mabao 2-1 dhidi ya Manchester City ulitosha kuweka matumaini hai kwa Spurs kunyakuwa taji lao la kwanza la Ligi Kuu toka mwaka 1961. Pochettinho alimzidi meneja wa Leicester City Claudio Ranieri katika kinyang’anyiro cha tuzo hiyo, kwani naye alikiongoza kikosi chake kushinda mechi tatu kati ya nne mwezi uliopita ambazo ni dhidi ya Liverpool, Manchester City na Norwich City. Guus Hiddink naye pia alikuwepo katika kinyang’anyiro hicho baada ya kuingoza Chelsea kufanya vyema huku golikipa wa Southampton Fraser Forster akitwaa tuzo ya mchezaji bora wa mwezi. Forster amefanikiwa kuzuia nyavu zake kutikiswa ukiwemo mchezo wa ugenini dhidi ya Arsenal na kuweka rekodi mpya ya klabu kwa kucheza dakika 708 bila kufungwa.

No comments:
Post a Comment