Sunday, March 13, 2016

PSG KUWAFUKUZIA HAZARD NA COURTOIS.

KLABU ya Paris Saint-Germain-PSG inadaiwa kujipa kutoa ofa kwa nyota wawili wa Chelsea baada ya kuwang’oa katika michuano ya Ligi ya Mabingwa Ulaya. Chelsea ambao wako katika hatihati ya kutofuzu michuano ya Ulaya msimu ujao kutokana na kiwango duni walichoonyesha msimu huu katika mechi zao za Ligi Kuu, wanaweza kupoteza nyota wake kadhaa na PSG wanataka kutumia mwanmya huo. Vinara hao wa Ligue 1 wana matumaini ya kuwapiga bao Real Madrid na kumnasa winga wao mahiri Eden Hazard pamoja na kipa namba moja Thianaut Courtois. PSG wanadaiwa kutaka kubadilisha kipa kutokana na Kevin Trapp kuonekana kutokidhi vigezo vya kuwa namba moja kwenye kikosi cha timu hiyo.

No comments:

Post a Comment