Tuesday, November 15, 2016

SCHWEINSTEIGER AANZA MIPANGO YA KUONDOKA OLD TRAFFORD.

KIUNGO wa Manchester United, Bastian Shweinsteiger amekutana na viongozi wa klabu ya Chicago Fire ikiwa ni katika harakati za kuondoka Old Trafford Januari mwakani. Nahodha huyo wa zamani wa kimataifa wa Ujerumani mwenye umri wa miaka 32, ameruhusiwa kufanya majadiliano na klabu zingine. Inadaiwa kuwa anataka kwenda kujiunga na klabu hiyo inayoshiriki Ligi Kuu ya Marekani-MLS kufuatia kukutana na kocha Veljko Paunovic mwishoni mwa wiki iliyopita. Schweinsteiger alirejea kufanya mazoezi na kikosi cha kwanza baada ya kulazimishwa kufanya mazoezi mwenyewe na Jose Mourinho.

No comments:

Post a Comment