KLABU ya Barcelona jana imeweka historia mpya ya kuwa timu ya kwanza kucheza pasi nyingi katika michuano ya Ligi ya Mabingwa Ulaya jana. Wakiwa tayari wameshafuzu wakiwa vinara w akundi C, Barcelona walishinda mabao 4-0 dhidi ya Borussia Monchengladbach, mabao yaliyofungwa na Lionel Messi na Arda Turan aliyefunga hat-trick. Katika mchezo huo Barcelona walicheza pasi 993 ikiwa ni nyingi zaidi kuliko timu yeyote toka rekodi hizo zilipoanza kutunzwa katika msimu wa 2003-2004. Mapema msimu huu, kipa wa Barcelona Marc-Adre ter Stegen aliweka rekodi mpya katika La Liga baada ya kutoa pasi zilizokamilika 51 kati ya 62 alizopiga dhidi ya Athletic Bilbao.

No comments:
Post a Comment