Thursday, December 15, 2016

EVERTON YAMUWANIA SCHNEIDERLIN.

KLABU ya Everton inadaiwa kuanza mazungumzo na Manchester United kwa ajili ya kumleta kiungo Morgan Schneiderlin Goodison Park kipindi cha Januari mwakani. Schneiderlin hajaanza katika mechi yeyote ya Ligi Kuu chini ya Jose Mourinho msimu huu na taarifa zinadai kuwa meneja huyo wa United anaweza kumruhusu Mfaransa huyo aondoke kiangazi kama atapata timu. Meneja wa Everton Ronald Koeman aliwahi kufanya kazi na Schneiderlin wakati wote wakiwa Southampton na sasa anataka kutenga kitita cha paundi milioni 24 ili aweze kuungana tena na mchezaji wake huyo wa zamani. Schneiderlin anapitia kipindi kigumu United kwasasa lakini kufanya kazi tena na Koeman inaweza kuwa hatua nzuri kwake ya kuendelea kuimarika zaidi.

No comments:

Post a Comment