KLABU ya Kashima Antlers imefanikiwa kutinga hatua ya fainali ya michuano ya Klabu Bingwa ya Dunia baada ya kuitandika Atletico Nacional kwa mabao 3-0 mapema leo. Katika mchezo huo mwamuzi Viktor Kassai wa Ukraine alitumia kwa mara ya kwanza mfumo mpya wa usaidizi wa picha za video-VAR ambao uko katika majaribio, kwa kutoa penati iliyowapa bao la kuongoza Kashima. Klabu ya Atletico ya Colombia ambao ni mabingwa wa kutoka Amerika Kusini-CONMEBOL walikwenda katika michuano hiyo huku wakiwa na majonzi kufuatia mkasa wa ajali ya ndege iliyoikuta timu ya Chopecoense mwishoni mwa uliopita. Chapecoense walikuwa wakilekea jijini Medellin kwenda kucheza na Atletico mchezo wa fainali ya mkondo wa kwanza wa michuano ya Copa Sudamericana kabla ya ajali hiyo ambayo iliua wachezaji 19 na kunusurika watatu pekee. Kashima ambao wanashiriki michuano hiyo kama timu mwenyeji sasa wansubiri kucheza na mshindi kati ya mabingwa wa Ulaya Real Madrid au mabingwa wa CONCACAF Club America ya Mexico.

No comments:
Post a Comment