Wednesday, December 14, 2016

RAMOS KUIKOSA NUSU FAINALI YA KLABU BINGWA YA DUNIA.

NAHODHA wa Real Madrid, Sergio Ramos ameondolewa katika mchezo wa nusu fainali ya michuano ya Klabu ya Dunia dhidi ya Club America utakaofanyika kesho. Meneja wa Madrid Zinedine Zidane amethibitisha kuwa nyota huyo wa kimataifa wa Hispania, hatakuwepo katika mchezo huo dhidi ya mabingwa hao wa CONCACAF baada ya kulalamika maumivu ya mguu wakati wakiwa safarini kwenda Japan. Akihojiwa na wanahabri, Zidane amesema Ramos hatacheza kwani alikuwa akijisikia maumivu wakati wakiwa njiani hivyo hatahatarisha afya yake. Ramos amekuwa mchezaji muhimu katika kikosi cha Madrid msimu huu akifunga mabao muhimu ambayo yameifanya timu hiyo kuendelea kuongoza La Liga kwa tofauti ya alama sita. Mabingwa hao wa Ulaya wataanza kampeni zao katika michuano hiyo dhidi ya klabu hiyo ya Mexico huko jijini Yokohama.

No comments:

Post a Comment