Wednesday, December 14, 2016

SUPER AFCON WATINGA BUNGENI ABUJA.

TIMU ya taifa ya ya wanawake ya Nigeria wameandamana nje ya bunge jijini Abuja wakidai bakshishi zao ambazo hazijalipwa. Wachezaji hao waliandamana bungeni hapo wakati rais Muhammadu Buhari akiwasili bungeni kwa ajili ya kuwasilisha bajeti yake katika kipindi cha mwaka ujao. Mabingwa wa Afrika baadae waliandamana tena mpaka katika makazi ya rais Buhari ambapo mmoja wa wasaidizi wake alitoka na kuwaambia wachezaji hao kuwa watalipwa katika kipindi kisichozidi siku mbili. Wachezaji wamegoma kutoka katika hoteli waliyofikia toka walipotoka katika michuano hiyo, mpaka hapo watakapolipwa bakshishi zao ambazo ni dola 17,500 kila mmoja. Taarifa kutoka jijini Abuja zimedai kuwa baada ya maelezo hayo waliyopata kutoka kwa msaidizi wa Rais Buhari, wachezaji walirejea hotelini kusubiri serikali itemize ahadi yake.

No comments:

Post a Comment