MASHABIKI wa Soka barani Afrika wanasubiri kwa hamu ratiba ya makundi ya michuano ya Kombe la Mataifa ya Afrika 2012.Ratiba ya upangaji makundi hayo ambayo yatachuana katika michuano hiyo iliyoandaliwa kwa pamoja kati ya Gabon na Equatorial Guinea inatarajiwa kufanyika katika jiji la Malabo ambao ni mji mkuu wa Equatorial Guinea Jumamosi hii.Macho na masikio vyote vitaelekea katika mji huo ambapo marais wa nchi zote mbili Ali Bongo wa Gabon na Teodoro Obiang Nguema wanatarajiwa kuhudhuria katika sherehe hizo.Bingwa mtetezi wa michuano hiyo Misri hawatakuwemo katika timu 16 zilizofuzu kucheza ambazo zitakuwa zikisubiri kwa hamu ratiba hiyo ili zijue zitacheza na nani katika safari ndefu ya kufukuzia ubingwa katika mshindano hayo yanayotarajiwa kufanyia mwakani.
No comments:
Post a Comment