BOLT ANAWEZA KUKIMBIA MITA 100 KWA SEKUNDE 9.4 - JOHNSON.
 |
Usain Bolt. |
MWANARIADHA nyota wa zamani wa Marekani ambaye pia amewahi kuwa bingwa mara nne wa michuano ya Olimpiki, Michale Johnson anaamini kuwa Usain Bolt anaweza kukimbia mita 100 kwa kutumia sekunde 9.4 lakini kama ataboresha aina ya ukimbiaji wake. Bolt mwenye umri wa miaka 25 alivunja rekodi yake mwenyewe akitumia muda wa sekunde 9.58 katika michuano ya dunia iliyofanyika jijini Berlin, Ujerumani. Johnson amesema kuwa mwanariadha huyo raia wa Jamaica anaweza kukimbia zaidi hapo lakini anatakiwa kufanya juhudi kubwa ikiwemo kubadilisha mbinu zake katika ukimbiaji. Nyota huyo wa zamani aliendelea kusema kuwa hata kama hataweza kufikia muda huo bado anafikiri Bolt anaweza kutetea ubingwa wake katika michuano ya olimpiki itakayofanyika baadaye mwaka huu. Bolt ambaye katika michuano hiyo pia atakuwa akitetea ubingwa wa mita 200 pamoja na mbio za kupokezana vijiti za mita 400 jijini London, alitangaza mapema jana kujitoa katika mashindano ya Diamond League yatakayofanyika jijini Monaco kutokana na majeraha yanayomsumbua.
No comments:
Post a Comment