Wednesday, September 5, 2012

AFC KUENDELEA KUMCHUNGUZA BIN HAMMAM.

SHIRIKISHO la Soka barani Asia-AFC bado linaendelea na uchunguzi dhidi ya rais wa shirikisho hilo aliyesimamishwa Mohamed Bin Hammam pamoja na muda wa kusimamishwa kumalizika Jana. AFC inafanya uchunguzi kufuatia tuhuma za matumizi mabaya ya fedha aliyofanya Bin Hammam kipindi akiwa kiongozi wa shirikisho hilo. Katika taarifa iliyotolewa na AFC imesema kuwa pamoja na siku za kusimamishwa kuisha jana, Bin Hammam mwenye miaka 63 ambaye ni raia wa Qatar atandelea kutumikia adhabu yake ya siku 90 kutojishughulisha na soka aliyopewa na Shirikisho la Soka la Dunia-FIFA . FIFA ilimfungia maisha Bin Hammam kujishughulisha na soka kutokana na makosa ya kutoa rushwa wakati alipokuwa akigombani nafasi ya urais wa shirikisho hilo mwaka uliopita lakini adhabu hiyo ilitenguliwa na Mahakama ya Kimataifa ua Usuluhishi wa Michezo Julai 19 mwaka huu. Baadae FIFA ilimfungia kwa siku 90 ili kuandaa ushahidi mpya juu ya tuhuma zinazomkabili Bin Hammam baada ya CAS kusema kuwa hakukuwa na ushahidi wa moja kwa moja kwamba mtuhumiwa alitoa rushwa. Bin Hammam alikana makosa yote hayo anayotuhumiwa na AFC na FIFA na kudai kuwa anajipanga na baadae atangaze hatua atakazozichukua kuhusiana na changamoto hizo zinazomkabili.

No comments:

Post a Comment