Monday, September 3, 2012
BRAZIL KUTUMIA JINA LA "BRAZUCA" KATIKA MIPIRA ITAKAYOTUMIKA KWENYE KOMBE LA DUNIA 2014.
SHIRIKISHO la Soka Duniani-FIFA limesema kuwa nchi ya Brazil imeamua kuupa jina la Brazuca mpira utakaotumika kwa ajili ya michuano ya Kombe la Dunia 2014 jina ambalo hutumika mara chache kuonyesha fahari ya taifa hilo lililopo Amerika ya Kusini. FIFA wamesema kuwa watu zaidi ya milioni moja walipiga kuchagua majina mbalimbali huku asilimia 70 ya watu hao walichagua jina hilo. Katika taarifa yake FIFA imesema kuwa jina hilo ni ishara ya hisia, fahari na ukarimu kwa wote nchi hiyo ikiwa kama kioo katika mchezo wa soka. Kampuni ya Ujerumani ya Adidas ambao ndio wasambazaji rasmi wa mipira ya Kombe la Dunia toka mwaka 1970, wamesema kuwa majina mengine mawili ambayo ni Bossa Nova na Carnavalesca ndio yalikuwa majina ya mwisho kupigiwa kura katika kinyang’anyiro hicho. FIFA waliendelea kusema kuwa hiyo ni mara ya kwanza mashabiki kushirikishwa moja kwa moja kutaja majina mpira utakaotumika kwa ajili ya michuano ya Kombe la Dunia, ambayo bado inatengenezwa na kujaribiwa na vilabu na vyama mbalimbali vya soka duniani kote.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)

No comments:
Post a Comment