Saturday, September 8, 2012
MERRITT AVUNJA REKODI YA DUNIA KATIKA MBIO ZA KURUKA VIUNZI.
MWANARIADHA nyota wa mbio fupi za kuruka viunzi za mita 110 amefanikiwa kuweka rekodi mpya ya dunia baada ya kutumia muda wa sekunde 12.80 katika michuano ya Diamond League iliyofanyika jijini Brussels, Ubelgiji. Merritt ambaye ni mshindi wa medali ya dhahabu katika michuano ya olimpiki alifanikiwa kuipita rekodi ya muda wa sekunde 12.87 iliyowekwa na Dyron Robles kutoka Cuba katika mashindano yaliyofanyika jijini Ostrana mwaka 2008. Nyota mwingine wa mbio fupi Usain Bolt kutoka Jamaica naye alifanikiwa kushinda mbio za mita 100 kwa kutumia muda wa sekunde 9.86 pamoja na kuanza taratibu huku rafiki yake Yohane Blake naye akishinda mbio za mita 200 kwa kutumia muda wa sekunde 19.54. Akihojiwa mara yam bio hizo Blake amesema kuwa alikuwa akitamani kuweka rekodi ya dunia katika mbio hizo lakini anaona uchovu umechangia lakini anaamini atakuwa katika kiwango kizuri tayari kwa ajili ya michuano ya mwakani.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)

No comments:
Post a Comment