
Monday, January 21, 2013
ATLETICO MADRID NA REALA MADRID ZAPUNGUZA PENGO NA BARCELONA.
KLABU za Atletico Madrid na majirani zao Real Madrid waliitumia vizuri nafasi ya kufungwa kwa Barcelona na Real Sociedad kupunguza pengo la alama wanazotofautiana katika La Liga kwa kushinda michezo yao ya jana. Madrid ambao walikuwa wakicheza kwa kiwango chao bora kabisa msimu huu walifanikiwa kuifunga Valencia kwa mabao 5-0 na kufanikiwa kupunguza pengo la alama kutoka alama 18 mpaka 15 walizotofautiana na vinara wa La Liga Barcelona. Barcelona walifungwa na Sociedad kwa mabao 3-2 katika mchezo uliochezwa Jumamosi na kutengua rekodi yao ya kutofungwa mchezo katika La Liga. Atletico nao walitumia vizuri rekodi yao ya kutofungwa nyumbani kwa kuifunga Lavante kwa mabao 2-0 mabao ambayo yalifungwa na Radamel Falcao na Adrian. Kocha wa Atletico Diego Simeone amesema amefurahishwa na matokeo hayo lakini amewataka wachezaji wake kutobweteka na kujipanga kwa ajili ya mchezo ujao wa robo fainali ya pili ya Kombe la Mfalme Alhamisi dhidi ya Real Betis ambapo timu hiyo itahitaji kulinda ushindi wake wa mabao 2-0 iliyopata katika mchezo wa kwanza.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment