Tuesday, March 19, 2013

KUNDI LA NYUKI LATISHIA KUSIMAMISHA MCHEZO BRAZIL.

MWISHONI mwa wiki iliyopita kundi ya nyuki ambao hawakujulikana walipotokea kidogo wazuie mchezo wa Ligi Kuu nchini Brazil usichezeke baada ya kujikusanya kundi katika mlingoti wa goli. Mchezo huo kati ya timu ya Ponte Preta na Atletico Sorocaba uliingia katika msukosuko huo baada ya kundi la nyuki kujikusanya katika mlingoti wa goli la Uwanja wa Moises Lucarelli na kadri muda wa kuanza pambano hilo ulipokuwa ukisogea ndivyo kundi la nyuki hao lilivyozidi kuongezeka na kuwa kubwa. Baadhi ya picha zilizopigwa uwanjani zinawaonyesha watu wa kikosi cha zimamoto waliovaa mavazi maalumu wakipanda katika ngazi kabla ya kuwapulizia mitungi ya kuzimia moto na baada ya kupuliza hewa ya petrol kuzunguka eneo hilo kabla ya mchezo huo kuanza. Kuchelewa kwa mechi hiyo ilikuwa ni faida ya wenyeji Ponte Preta ambao waliibuka na ushindi wa mabao 2-0 na kuendelea kung’ang’ania katika nafasi ya pili ya msimamo wa ligi ya nchi hiyo wakiwa na alama sawa na vinara Sao Paulo baada ya michezo 12 kuchezwa.

No comments:

Post a Comment