Tuesday, March 19, 2013

OWEN ATANGAZA KUTUNDIKA DARUGA.

MSHAMBULIAJI nyota wa zamani wa kimataifa wa Uingereza, Michael Owen ametangaza leo kustaafu rasmi soka ifikapo mwishoni mwa msimu huu. Owen mwenye umri wa miaka 33 alitangza azma yake hiyo katika mtandao wake binafsi kwa kudai kuwa anadhani wakati umefika wa kutundika daruga zake. Nyota huyo alianza kucheza katika kikosi cha kwanza Liverpool akiwa na umri wa miaka 17 na pia amewahi kucheza katika vilabu vya Real Madrid, Newcastle United, Manchester United na klabu yake ya sasa Stoke City. Mshambuliaji huyo ambaye amewahi kushinda tuzo ya mchezaji bora barani Ulaya mwaka 2001 amecheza mechi 89 za kimataifa akiwa na kikosi cha Uingereza na kufunga mabao 40 lakini maisha yake ya soka yamekuwa katika misukosuko kutokana na majeruhi ya mara kwa mara ambayo yamekuwa yakimsumbua. Owen aliwashukuru wale wote ambao wamekuwa karibu yake wakiwemo wachezaji, makocha na marafiki zake katika kipindi chote alichokuwa akicheza.

No comments:

Post a Comment