
Tuesday, April 2, 2013
NASRI AMTUHUMU KREONKE KUHUSU KUONDOKA KWAKE ARSENAL.
KIUNGO wa zamani wa klabu ya Arsenal, Samir Nasri amemtuhumu mmiliki wa klabu hiyo Stan Kroenke kumuuza Manchester City kwasababu alikuwa akitaka fedha kauli ambayo itazorotesha zaidi uhusiano wake na waajiri wa zamani. Meneja wa Arsenal, Arsene Wenger siku zote amesisitiza kuwa hakuwepo katika msukumo wowote wakati anamuuza Nasri kwenda City kwa ada ya paundi milioni 24 Agosti mwaka jana, pamoja na kwamba kiungo huyo wa Ufaransa alikuwa amebakisha mwaka mmoja katika mkataba wake. Nasri amesema Wenger alimwambia kuwa kama Cesc Fabregas ataondoka yeye atabakia lakini Kroenke alikuwa akihitaji fedha ndio maana akaamua kuondoka. Kiungo huyo alimalizia kuwa hajuti kujiunga na City na kuondoka kwake Arsenal ni kwasababu za kimichezo sio kifedha kama wengi wanavyodai.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment