
Thursday, May 2, 2013
AL KHALIFA ATEULIWA KUWA MJUMBE WA KAMATI YA UTENDAJI FIFA.
SHIRIKISHO la Soka barani Asia limemchagua Sheikh Salman Bin Ebrahim Al Khalifa kuwa mjumbe wa kamati ya utendaji ya Shirikisho la Soka Duniani-FIFA katika uchaguzi uliofanyika Malaysia. Al Khalifa ambaye ni raia wa Bahrain alifanikiwa kupata kura 28 katika kura 46 zilizopigwa ambapo alimshinda Hassan Al Thawadi wa Qatar aliyepata kura 18. Al Khalifa amewahi kuikosa nafasi hiyo ya juu kabisa ya maamuzi ya FIFA kwa kura chache baada ya kuzidiwa na aliyekuwa rais wa AFC Mohamed Bin Hammam kwa kura 23 kwa 21 mwaka 2009. AFC pia imemteua Al Khalifa kugombea nafasi ya urais wa shirikisho kwa kipindi kingine cha miaka miwili.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment