Friday, May 3, 2013

BRAZIL KUFUNGA MTANDAO WA INTERNET KATIKA VIWANJA VITAKAVYOTUMIKA KOMBE LA DUNIA 2014.

MASHABIKI wa soka watakaohudhuria michuano ya Kombe la Dunia 2014 nchini Brazil wanatajiwa kutopata matatizo ya mtandao pindi watakapokuwa uwanjani baada ya serikali ya nchi hiyo kuamua kuweka mitandao katika viwanja vyote vitakavyotumika kwa ajili ya michuano hiyo. Kila kiwanja kati ya 12 vitakavyotumika kwa ajili ya michuano hiyo ya 32 itatengewa mikondo miwili ya GB 50 ya mtandao kwa ajili ya kuwahudumia mashabiki watakaokuwa uwanjani kwa muda huo. Waziri wa mawasiliano wa nchi hiyo Paulo Bernardo amesema kiwango cha watakachikiweka ni kikubwa kiasi ambacho hadhani kama watu watakaohudhuria wataweza hata kutumia moja ya tatu ya mtandao huo. Bernardo amesema kwa kujitapa huku akimtupia madongo katibu mkuu wa Shirikisho la Soka Duniani FIFA Jerome Valcke kuwa hata kiongozi huyo hataweza kufikia kiwango hicho cha kutumia mtandao kama akiamua kutoa kauli za kuishambulia nchi hiyo. Valcke ameingia mgogoro na serikali ya Brazil katika kipindi cha karibuni baada ya kuishambulia nchi hiyo kwa maandalizi yake ya kusuasua katika viwanja na miundo mbinu ambayo itatumika kwa ajili ya michuano hiyo.

No comments:

Post a Comment