
Thursday, May 2, 2013
MAJERUHI SIO SABABU YA KUMUACHA MESSI - VILANOVA.
MENEJA wa klabu ya Barcelona, Tito Vilanova amebainisha kuwa majeruhi sio sababu ya kukosekana kwa mshambuliaji nyota wa klabu hiyo Lionel Messi katika mchezo wa mkondo wa pili wa nusu fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya dhidi ya Bayern Munich. Mshambuliaji huyo wa kimataifa wa Argentina aliwashangaza mashabiki wa timu hiyo baada ya kuondolewa katika kikosi kilichoanza dhidi ya Bayern huku wengi wakidhani majeruhi ya msuli wa paja ndio chanzo kikubwa cha kukosekana kwake. Hata hivyo kwa mujibu wa Vilanova majeruhi halikuwa tatizo la kumuacha Messi na kudai kuwa angeweza kumpa nafasi nyota huyo kuingia katika kipindi cha pili kama angedhani kikosi chake kilikuwa na nafasi ya kufika fainali. Vilanova amesema Messi hakuwa mgonjwa kama watu wanavyofikiri lakini alikuwa hajisikii vyema hivyo alifikiri kwamba kwa hali aliyokuwa nayo asingeweza kuisaidia timu hiyo kwa muda ule.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment