SHIRIKISHO la Soka Duniani-FIFA limemfungia mjumbe wake wa kamati ya utendaji Vernon Manilal Fernando wa Sri Lanka kwa miaka nane kwa tabia zisizo za maadili. Kamati ya maadili ya FIFA ikiongozwa na mwenyekiti wake Hans-Joachim Eckert ambayo ilikuwa ikisikiliza shauri hilo kwa siku mbili, imemkuta Fernando na hatia ya kukiuka kanuni za maadili ya FIFA. Fernando alichaguliwa mjumbe wa kamati ya utendaji wa shirikisho hilo mwaka 2011 katika mkutano ambao ndio uliomchagua Sepp Blatter kwa mara nyingine kuongoza FIFA. Fernando ni rafiki wa karibu na mjumbe wa zamani wa kamati ya utendaji ya FIFA na rais wa Shirikisho la Soka la Asia, Mohamed Bin Hammam ambaye amefungiwa maisha kwa kujihusisha na rushwa mwaka 2011.
No comments:
Post a Comment