Alvaro Vadillo akichuana na Pepe katika mojawapo ya mechi za La Liga.
KLABU ya Arsenal imepanga kuongeza juhudi za kulisajili kinda la miaka 18 ambaye anatambulika kama Cristiano Ronaldo mpya ili kuhakikisha hawazidiwi hesabu na mahasimu wao wa London Tottenham Hotspurs. Kinda huyo aitwaye Alvaro Vadillo anayecheza alikuwa akifuatiliwa na vilabu vingi vikubwa barani Ulaya lakini inaonekana Spurs na Arsenal sasa wameingia katika vita ya kumsajili nyota huyo. Kocha wa Arsenal, Arsene Wenger yuko katika shinikizo kutoka kwa mashabiki wakitaka asajili wachezaji wengine kabla ya msimu mpya haujaanza wakati Spurs ambao tayari wameshavunja rekodi yao ya usajili mara mbili katika kipindi hiki cha majira ya kiangazi wanategemea kupata kiasi cha paundi milioni 100 kwa mauzo ya Gareth Bale kwenda Real Madrid. Winga huyo wa kimataifa wa Hispania amekuwa akifananishwa na nyota wa Madrid Ronaldo kutokana na jinsi anavyotuliza mpira, chenga na jinsi anavyokokota akiwa katika wingi ya kushoto. Agosti mwaka 2011 akiwa na umri wa miaka 16 na miezi 11 aliweka historia ya kuwa mchezaji mdogo zaidi kucheza La Liga baada ya Real Betis kumpandisha katika timu ya wakubwa katika ushindi wa bao 1-0 iliyopata timu hiyo dhidi ya Granada. Octoba mwa huohuo Manchester United waliripotiwa kutoa ofa ya paundi milioni 2.5 kwa ajili ya kumsajili lakini walikataliwa kufuatiwa kocha Betis kudai kuwa atakuwa na thamani zaidi ya hiyo katika kipindi cha muda mfupi.
No comments:
Post a Comment