PAMOJA na utata unaoendelea, Isha Johansen amethibitishwa kuwa rais mpya wa Shirikisho la Soka nchini Sierra Leone kutokana na kupita bila kupigwa katika uchaguzi baada ya wagombea wengine kuenguliwa katika kinyang’anyiro hicho kwa kukosa vigezo. Isha mwenye umri wa miaka 48 anakuwa mwanamke wa pili kuwa kiongozi katika ulimwengu wa soka pamoja na Lydia Nsekera ambaye ni rais wa Shirikisho la Soka nchini Burundi. Kazi ya kwanza Johansen akiwa madarakani ni kuhakikisha ligi ya soka ya nchi hiyo inaendelea baada ya vilabu kugomea kutokana na wagombea watatu wa nafasi hiyo kufungiwa. Uchaguzi wa Sierra Leone umekuwa ukikumbwa na utata kwa karibu mwaka mzima sasa na bado umeendelea kuzua mjadala juu ya wajumbe wenye haki ya kupiga kura katika uchaguzi ambao Johansen ameshinda.
No comments:
Post a Comment