MCHEZAJI nyota wa mchezo wa baseball anayelipwa zaidi, Alex Rodriguez kutoka Marekani amedai kuwa anapambana kwa ajili ya maisha yake kufuatiwa yeye pamoja na wachezaji wenzake 12 kufungiwa kutokana na kashfa ya kutumia dawa za kuongeza nguvu. Ligi Kuu ya Baseball nchini humo imemfungia nyota huyo anayecheza katika timu ya New York Yankees kwa michezo 211 adhabu ambayo itamalizika mwishoni mwa msimu wa mwaka 2014. Rodriguez mwenye umri wa miaka 38 ni mmoja kati wachezaji wachache ambao walikuwa wakihusihwa na kliniki ya Florida iliyofungwa kutokana na tuhuma za kutoa dawa za kusisimua misuli ambazo zimepigwa marufuku. Nyota huyo ambaye anajulikana zaidi kama A-Rod amesema atakata rufani kupinga adhabu aliyopewa ambapo atakuwa akiendelea kucheza wakati rufani yake ikisikilizwa.
No comments:
Post a Comment