Monday, August 5, 2013

RONALDO AKATAA KUMJIBU MOURINHO KWA KAULI YAKE YA KUMPONDA.

MSHAMBULIAJI nyota wa klabu ya Real Madrid ya Hispania Cristiano Ronaldo amekataa kujibu kauli ya Jose Mourinho aliyotoa dhidi yake zikiwa zimebakia siku mbili kabla ya Madrid na Chelsea kukwaana uso kwa uso huko Miami, Marekani. Mourinho ambaye anainoa Chelsea alimpuuza nyota huyo ambaye wote wanatoka Ureno kwa kumuelezea mshambuliaji nyota wa zamani wa kimataifa wa Brazil na klabu za Barcelona na Inter Milan ambaye wanatumia jina moja kwamba ndio Ronaldo wa kweli wakati akihojiwa na luninga ya ESPN. Mourinho amesema amekuwa kocha rasmi mwaka 2000 lakini kabla ya hapo alikuwa kocha msaidizi katika vilabu vikubwa akifundisha wachezaji wengi nyota kama Ronaldo de Lima, Rivaldo, Luis Figona hata Pep Guardiola wakati akiwa na umri mdogo. Akihojiwa kuhusiana na kauli ya kocha wake huyo wa zamani, Ronaldo amesema kuna vitu katika maisha ambavyo havipaswi kutajwa na hatatoa kauli yake kuhusu hilo kutokana na sababu nyingi alizonazo. Ronaldo amesema siku zote amekuwa akijaribu kuheshimu makocha wote wanaomfundisha na kujaribu kusoma kitu kutoka kwao hivyo hivyo atapendelea zaidi kujaribu kukumbuka mazuri ya Mourinho.

No comments:

Post a Comment