Monday, January 13, 2014

BAFANA BAFANA KUMWAGIWA ZAWADI WAKICHUKUA CHAN.

WAZIRI wa michezo wa Afrika Kusini Fikile Mbalula amedai kuwa timu ya taifa ya nchi hiyo, Bafana Bafana watapewa zawadi nono kama wakifanikiwa kunyakuwa la michuano ya Afrika kwa wachezaji wanaocheza ndani bara hili ijulikayo kama CHAN. Bafana Bafana ilianza vyema kampeni zao katika michuano ya kwa kuifunga Msumbiji katika mchezo wa ufunguzi wa kundi A na kuendeleza rekodi yao ya ushindi kwa silimia 100 dhidi ya majirani zao hao. Akihojiwa Mbalula amesema anachojua yeye kama timu hiyo ikifanikiwa kunyakuwa michuano hiyo ya CHAN kuna zawadi nono itafuatia lakini pia hata kama hawatashinda kwa kushika nafasi ya pili au tatu watakaa chini na Chama Cha Soka cha nchi hiyo,SAFA ili kuangalia zawadi ya kuwpaa kwa juhudi zao. Michuano hiyo iliendelea jana ambapo kwa mechi za kundi B ambapo Zimbabwe ilishindwa kutambiana na Morocco kwa kwenda ya bila ya kufungana huku Uganda ikiibugiza Burkina Faso kwa mabao 2-1. Mechi za leo za kundi C zitakutanisha timu za Ghana na Congo katika mchezo wa kwanza ukifuatia na mwingine utakaozikutanisha timu za Libya na Ethiopia ambapo mechi zote zitachezwa katika uwanja wa Free State huko Mangaung.

No comments:

Post a Comment