Thursday, January 9, 2014

FERDINAND, VIDIC, EVRA KATIKA KIKANGO UNITED.

MENEJA wa klabu ya Manchester United, David Moyes anapanga kukisuka upya kikosi cha timu hiyo ambapo baadhi ya wachezaji wanatarajiwa kuonyeshwa mlango wa kutokea. United kwasasa iko katika mgogoro baada ya kupoteza michezo mitatu iliyocheza mwaka huu na Moyes anataka kupunguza baadhi ya wachezaji ambao hawatakiwi na hawana furaha ili kujaribu kurejesha makali ya timu hiyo. Mojawapo ya wachezaji wanaotarajiwa kuonyeshwa mlango wa kutokea ni pamoja na Rio Ferdinand, Nemanja Vidic na Patrice Evra huku Javier Hernandez, Nani, Anderson, Alex Buttner na Anders Lindegaard nao wakiwa katika hatihati. Mbali na hayo pia kumekuwa na hofu kuhusu Wayne Rooney kukataa kusaini mkataba mpya na Robin van Persie kushindwa kucheza katika kiwango kikubwa toka Moyes aliposhika mikoba ya kuinoa United.

No comments:

Post a Comment