DAKTARI mkuu wa Shirikisho la Soka Duniani, FIFA, Jiri Dvorak ameahidi kuwa wachezaji wote watakaoshiriki michuano ya Kombe la Dunia mwaka huu watapimwa vipimo vya madawa ya kusisimua misuli kabla ya mechi ya ufunguzi. FIFA imezitaka timu 32 zilizofuzu michuano hiyo itakayochezwa nchini Brazil kutuma ratiba zao kuanzia Machi mosi ili kutoka nafasi kwa shirikisho hilo kuwapima wachezaji wote. Dvorak amefafanua kuwa wachezaji na timu hazitajua lini wapimaji watafika lakini ameahidi kuwa hakuna atakayekosa vipimo hivyo kabla ya mchezo wa kwanza wa ufunguzi ambao utakzikutanisha wenyeji Brazil na Croatia Juni 12. Dvorak aliendelea kudai anafurahishwa na watu kutaka kujua lini wataanza zoezi hilo kwasababu ni jambo ambalo hawataliweka hadharani na wataamua kuanza kupima muda wowote mahali popote wakati watakapoamua kufanya hivyo.

No comments:
Post a Comment