Wednesday, March 5, 2014

ABIDAL ALAZWA TENA KWA SIKU MBILI.

KLABU ya Monaco imedai kuwa beki wake Eric Abidal alilazwa kwa muda wa siku mbili hospitalini kufuatia kupata maambukizi ya virusi. Beki huyo wa kimataifa wa Ufaransa alitumia muda wa saa 48 akifanyiwa vipimo katika hospitali ya Princess Grace iliyopo Monaco kama sehemu ya tahadhari kutokana na maradhi ya saratani yaliyowahi kumpata kipindi cha nyuma. Abidal mwenye umri wa miaka 34 aligundulika kuwa saratani ya ini mwaka 2011 na kufanyiwa upasuaji wa kupandikiza ini jingine mwaka uliofuatia ili kutibu tatizo lake hilo. Hata hivyo taarifa ya klabu hiyo iliendelea kudai kuwa beki huyo aliruhusiwa na atafanya mazoezi na wenzake kama kawaida.

No comments:

Post a Comment