BAADA ya kushindwa kupata mafanikio katika timu ya wanaume, Afrika Kusini imemua kuahamishia nguvu zake kwa timu ya taifa ya wanawake kwa kutuma maombi ya kuandaa michuano ya Kombe la dunia la Wanawake mwaka 2019. Nchi hiyo tayari imeshapata haki ya kuandaa michuano hiyo kwa vijana chini ya umri wa miaka 20 mwaka 2016 ikiwa ni mara ya kwanza michuano mikubwa ya wanawake kuandaliwa katika bara la Afrika. Pamoja na kukabiliwa na ushindani kutoka kwa mabingwa wa Dunia kwa wanawake Japan, rais wa Chama Cha Soka cha Afrika Kusini Danny Jordaan anaamini kuwa wanaweza kupata nafasi kutokana na uzoefu wao wa kuandaa michuano mikubwa. Jordaan pia alimtangaza Vera Pauw raia wa Ureno kuwa kocha mpya wa timu ya taifa ya wanawake, Banyana Banyana huku jukumu lake la kwanza likiwa ni kuhakikisha timu hiyo inafuzu michuano ya mwaka 2015 itakayofanyika Canada.

No comments:
Post a Comment