RAIS wa klabu ya Paris Saint-Germain-PSG Nasser Al-Khelaifi amebainisha kuwa wanatarajia kumpatia mkataba mpya kocha wa timu hiyo Laurent Blanc. Kocha huyo wa zamani wa timu ya taifa ya Ufaransa alichukua mikoba ya kuinoa PSG baada ya timu hiyo kuhangaika kwa muda kutafuta mbadala wa Carlo Ancelotti aliyekwenda kuinoa Real Madrid katika majira ya kiangazi mwaka jana. Kumekuwa na tetesi kuwa PSG wanamtaka Arsenal Wenger kuchukua nafasi ya Blanc mwenye umri wa miaka 48 mwishoni mwa msimu huu. Hata hivyo tetesi hizo zimekanushwa vikali na bilionea huyo wa Qatar ambaye anataka Blanc aendelee kuinoa klabu hiyo. PSG kwasasa wako katika nafasi nzuri ya kutetea taji lao la Ligi Kuu nchini Ufaransa huku pia wakiwa wametinga robo fainali ya michuano ya Ligi ya Mabingwa Ulaya.

No comments:
Post a Comment