Friday, March 14, 2014

MWENYEKITI WA AL AHLY ABWAGA MANYANGA.

MWENEKITI wa klabu ya Al Ahly ya Misri Hassan Hamdi ameachia ngazi wadhifa wake huo kutokana na sheria mpya inayoweka ukomo wa uongozi iliyowekwa na wajumbe wa bodi ya klabu hiyo. Sheria hiyo mpya ambayo imepangwa kupelekwa katika Wizara ya Michezo ya nchi hiyo ili kupata baraka zao, itakuwa ikizuia wajumbe kukaa madarakani kwa zaidi mihula miwili ambayo ni miaka nane. Hamdi tayari ameshakaa madarakani kwa vipindi viwili hivyo ameamua kukaa kando kabla ya uchaguzi wa klabu hiyo Machi 28 mwaka huu. Klabu hiyo pia itachagua wakurugenzi wapya wa bodi katika uchaguzi huo.

No comments:

Post a Comment