Tuesday, March 11, 2014

NITAULINDA UTAJIRI WA HISTORIA WA AC MILAN.

MENEJA wa klabu ya AC Milan, Clarence Seedorf ameapa kuheshimu utajiri wa historia iliyinayo klabu hiyo katika michuano ya Ligi ya Mabingwa Ulaya kwa kuingoza kutinga hatua ya robo fainali leo usiku. Seedorf anakabiliwa na kibarua kizito kama atataka kufanya hivyo baada ya kuambulia kipigo cha bao 1-0 katika mchezo wao wa mkondo wa kwanza dhidi ya Atletico Madrid uliochezwa katika Uwanja wa San Siro mwezi uliopita. Kocha huyo amesema ameshakuwa katika sehemu hiyo ya kutopewa nafasi wakati akiwa mchezaji lakini waliweza kujikwamua na kushinda mataji muhimu. Seedorf aliendelea kudai kuwa anajua Atletico ndio wanaopewa nafasi kubwa ya kusonga mbele katika mchezo huo lakini kwa mwazo yake anaona mchezo bado uko wazi na timu yoyote inaweza kusonga mbele.

No comments:

Post a Comment